Tuesday, November 15, 2011

Eng. ATHUMAN FUKO (Mdau wa Blog) & Dr. HALIMA WEDDING

EVENT: WEDDING & RECEIPTION
COLOR: AQUA BLUE & GRAY
VENUE: TAZARA
MC: KENYATA (KENNY CHAPOMBE)
DATE: 12 NOVEMBER 2011

 Mr.&Mrs. Fuko siku ya ndoa yao iliyofungwa Mombasa Kenya siku ya tarehe 09 Novemba 2011

 Wanandoa siku ya Receiption yao iliyofanyika siku ya tarehe 12 Novemba 2011 katika ukumbi wa Tazara Dar es Salaam. kwakweli They made it!!

 Maharusi wetu wakifungua muziki, kwa pozi la aina yake. mi mkia tu huo wa tausi. weraweraaa!!!\

 Maharusi katika picha ya familia.

Bi harusi wetu akiwa saluni mambo ya Anet Salon TMK Dar.

Wednesday, October 26, 2011

MAAJABU 7 YA DUNIA!!

 
1. Piramidi za Giza ni kati ya majengo yanayojulikana zaidi duniani. Ziko kando la bonde la Nile   karibu na mji wa Giza takriban 15 km kutoka Kairo katika Misri. Piramidi hizi ni mabaki ya eneo kubwa la makaburi ya enzi za Misri ya Kale. Wafalme na maafisa wa juu walizikwa hapa. Piramidi za Giza zahesabiwa kati ya maajabu ya dunia ya kale. Piramidi tatu kubwa zaitwa kufuatana na mafarao au wafalme wa Misri waliozikwa ndani yao: piramidi za Cheops, Khefren na Mykerinos.


 2. Bustani Zenye Kuning’inia za Babylon au Hanging Gardens of Babylon” kwa Kiingereza.
Bustani hizo zilijengwa katika mji wa zamani wa Babylon (au Babeli), karibu na jiji ambalo leo linajulikana kama Al Hillah, jimbo la Babil, nchini Iraq. Maajabu hayo yalikuwa pia yakijulikana kama “Bustani Zenye Kuning’inia za Semiramis”. Semiramis anasemekana alikuwa ni malkia maarufu aliyeishi zama hizo. Kwa ufahamisho tu, mji wa Babylon, leo hii umebaki magofu tu, ambapo Al Hillah, ulio kando ya mto Euphrates (kilomita 100 kusini mwa Baghdad), una watu wapatao 400,000. Kwa nini bustani hizo zilipewa jina hilo? Ni kwa kuwa zilikuwa zimepandwa juu ya mapaa ya majengo, hususani maghorofa, katika vibaraza vya pembeni na kwenye mapaa kiasi kwamba miti hiyo ambayo matawi yake yalikuwa yanatokeza au kuning’inia pembeni mwa majengo, ikazaa maneno “Bustani Zenye Kuning’inia za Babylon”
Kuna mdau aliniuliza ni wapi ipo bustani ya babylon?? nikaamua kuisaka kule ilipo na kumtundikia humu ili apate kuiona. Mchana mwema!!

Wednesday, October 19, 2011

Picha za Misikiti ya kihistoria katika Mji Mtukufu wa Madina.

 Msikiti wa Mtume (Masjid Nabawi), kwa mara ya kwanza ulijengwa mwaka 622 AD, kuta zake zilitengenezwa kwa matofali ya tope na paa za msikiti huo zilikuwa ni magogo ya mitende.

MSIKITI WA GHAMAMA
Sehemu au mahala ulipo Msikiti wa Ghamama(Masjid Ghamama) leo hii,ilikuwa ni eneo la wazi wakati wa Mtume (s.a.w.w) ambapo mara nyingi sala ya (Eid ul-Fitr na Eid ul- Adh-ha) ilikuwa ikifanyika.Siku hizi Msikiti wa Ghamama uko karibu sana na Msikiti wa Mtume (s.a.w.w) kutokana na upanuzi wa Msikiti wa Mtume (s.a.w.w). Neno "Ghamama" kwa kiarabu lina maana ya "Mawingu".Msikiti huu umepewa jina hili kwa sababu ni mahali ambapo Mtume (s.a.w.w) alisimama na kuswali kwa ajili ya kuomba Mvua ambapo baada ya sala hiyo mvua ilinyesha kwa kiwango cha kutosha.

  MSIKITI WA QUBA


Pindi Mtume Muhammad (s.a.w.w) alipo hamia Madina,baada ya kufika, sehemu ya kwanza kabisa aliyotia nanga ilikuwa ni Babi Amr bin Awf,na alikaa Quba kwa muda wa siku tatu.Mtume (s.a.w.w) alijenga msikiti sehemu hiyo,na huo ndio msikiti wa kwanza kujengwa katika Mji wa Madina.Msikiti huo ulipewa jina la:Msikiti wa Quba (Masjid Qubaa).
Umbali uliopo kutoka Msikiti wa Mtume (s.a.w.w) hadi msikiti wa Quba ni kilomita 3.25.


  Mtume (s.a.w.w) alipohamia Madina akitokea Makka,akiwa bado njiani katika safari hiyo,alipofika maeneo hayo,alikaa kwa mapumziko mafupi mahala hapa (ambapo leo hii ndipo ulipo msikiti wa Ijumaa) kwa ajili ya kutekeleza sala ya Ijumaa kabla ya kuanza upya safari yake kuelekea sehemu ambayo ataishi katika mji wa Madina.
Kuna miskiti mingine mingi sana ya kihistoria katika Mji Mtukufu wa Madina,kama vile msikiti wa Amirul-Muminina Ali bin Abi Talib (a.s),Msikiti wa Abubakr,na Umar bin Khattab
MSIKITI WA MIQAT

 Msikiti wa miqat (Masji Meeqat) uko katika eneo la Dhul-Hulayfa,msikiti huu unajulikana pia kwa jina la Abyar Ali.Ni mahali ambapo Mahujaji huja kutoka Madina kwa ajili ya kufanya Umrah au Hajj ambapo huvaa Ihram kabla ya kuelekea Makka.
Umbali uliopo toka Msikiti wa Mtume (s.a.w.w) hadi msikiti wa Meeqat,ni kilomita 9


Msikiti wa Qibla mbili (Masjid Al-Qibla'tain),hujulikana kwa jina hilo kwa kuwa ni msikini ambao Qibla ilibadilika kutoka Yerusalemu kwenda Makka(ya Ka'aba).
Umbali uliopo toka Msikiti wa Mtume (s.a.w.w) hadi msikiti wa Qibla mbili, ni kilomita 3.5.

Picha zote kwa hisani ya www.imamtaqee.com


Je wadau mnakumbuka hii ilikua lini??? Rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ally Hassan Mwinyi na The Late Michael Jackson (Mfalme wa Pop) alipotembelea Tanzania miaka ya 199...!!