Wednesday, October 26, 2011

MAAJABU 7 YA DUNIA!!

 
1. Piramidi za Giza ni kati ya majengo yanayojulikana zaidi duniani. Ziko kando la bonde la Nile   karibu na mji wa Giza takriban 15 km kutoka Kairo katika Misri. Piramidi hizi ni mabaki ya eneo kubwa la makaburi ya enzi za Misri ya Kale. Wafalme na maafisa wa juu walizikwa hapa. Piramidi za Giza zahesabiwa kati ya maajabu ya dunia ya kale. Piramidi tatu kubwa zaitwa kufuatana na mafarao au wafalme wa Misri waliozikwa ndani yao: piramidi za Cheops, Khefren na Mykerinos.


 2. Bustani Zenye Kuning’inia za Babylon au Hanging Gardens of Babylon” kwa Kiingereza.
Bustani hizo zilijengwa katika mji wa zamani wa Babylon (au Babeli), karibu na jiji ambalo leo linajulikana kama Al Hillah, jimbo la Babil, nchini Iraq. Maajabu hayo yalikuwa pia yakijulikana kama “Bustani Zenye Kuning’inia za Semiramis”. Semiramis anasemekana alikuwa ni malkia maarufu aliyeishi zama hizo. Kwa ufahamisho tu, mji wa Babylon, leo hii umebaki magofu tu, ambapo Al Hillah, ulio kando ya mto Euphrates (kilomita 100 kusini mwa Baghdad), una watu wapatao 400,000. Kwa nini bustani hizo zilipewa jina hilo? Ni kwa kuwa zilikuwa zimepandwa juu ya mapaa ya majengo, hususani maghorofa, katika vibaraza vya pembeni na kwenye mapaa kiasi kwamba miti hiyo ambayo matawi yake yalikuwa yanatokeza au kuning’inia pembeni mwa majengo, ikazaa maneno “Bustani Zenye Kuning’inia za Babylon”




Kuna mdau aliniuliza ni wapi ipo bustani ya babylon?? nikaamua kuisaka kule ilipo na kumtundikia humu ili apate kuiona. Mchana mwema!!

No comments: