Wednesday, October 19, 2011

Picha za Misikiti ya kihistoria katika Mji Mtukufu wa Madina.

 Msikiti wa Mtume (Masjid Nabawi), kwa mara ya kwanza ulijengwa mwaka 622 AD, kuta zake zilitengenezwa kwa matofali ya tope na paa za msikiti huo zilikuwa ni magogo ya mitende.

MSIKITI WA GHAMAMA
Sehemu au mahala ulipo Msikiti wa Ghamama(Masjid Ghamama) leo hii,ilikuwa ni eneo la wazi wakati wa Mtume (s.a.w.w) ambapo mara nyingi sala ya (Eid ul-Fitr na Eid ul- Adh-ha) ilikuwa ikifanyika.Siku hizi Msikiti wa Ghamama uko karibu sana na Msikiti wa Mtume (s.a.w.w) kutokana na upanuzi wa Msikiti wa Mtume (s.a.w.w). Neno "Ghamama" kwa kiarabu lina maana ya "Mawingu".Msikiti huu umepewa jina hili kwa sababu ni mahali ambapo Mtume (s.a.w.w) alisimama na kuswali kwa ajili ya kuomba Mvua ambapo baada ya sala hiyo mvua ilinyesha kwa kiwango cha kutosha.

  MSIKITI WA QUBA


Pindi Mtume Muhammad (s.a.w.w) alipo hamia Madina,baada ya kufika, sehemu ya kwanza kabisa aliyotia nanga ilikuwa ni Babi Amr bin Awf,na alikaa Quba kwa muda wa siku tatu.Mtume (s.a.w.w) alijenga msikiti sehemu hiyo,na huo ndio msikiti wa kwanza kujengwa katika Mji wa Madina.Msikiti huo ulipewa jina la:Msikiti wa Quba (Masjid Qubaa).
Umbali uliopo kutoka Msikiti wa Mtume (s.a.w.w) hadi msikiti wa Quba ni kilomita 3.25.


  Mtume (s.a.w.w) alipohamia Madina akitokea Makka,akiwa bado njiani katika safari hiyo,alipofika maeneo hayo,alikaa kwa mapumziko mafupi mahala hapa (ambapo leo hii ndipo ulipo msikiti wa Ijumaa) kwa ajili ya kutekeleza sala ya Ijumaa kabla ya kuanza upya safari yake kuelekea sehemu ambayo ataishi katika mji wa Madina.
Kuna miskiti mingine mingi sana ya kihistoria katika Mji Mtukufu wa Madina,kama vile msikiti wa Amirul-Muminina Ali bin Abi Talib (a.s),Msikiti wa Abubakr,na Umar bin Khattab




MSIKITI WA MIQAT

 Msikiti wa miqat (Masji Meeqat) uko katika eneo la Dhul-Hulayfa,msikiti huu unajulikana pia kwa jina la Abyar Ali.Ni mahali ambapo Mahujaji huja kutoka Madina kwa ajili ya kufanya Umrah au Hajj ambapo huvaa Ihram kabla ya kuelekea Makka.
Umbali uliopo toka Msikiti wa Mtume (s.a.w.w) hadi msikiti wa Meeqat,ni kilomita 9


Msikiti wa Qibla mbili (Masjid Al-Qibla'tain),hujulikana kwa jina hilo kwa kuwa ni msikini ambao Qibla ilibadilika kutoka Yerusalemu kwenda Makka(ya Ka'aba).
Umbali uliopo toka Msikiti wa Mtume (s.a.w.w) hadi msikiti wa Qibla mbili, ni kilomita 3.5.

Picha zote kwa hisani ya www.imamtaqee.com



1 comment:

kighumi said...

Ndugu zangu wapendwa, nimeona niwapostie picha hizi za misikiti ya kihistoria ili iweze kuwapa hamasa wale wote waliosahau misikiti, aidha kwa kuwa wamebanwa na shughuli mbalimbali za maisha ya kila leo. hivyo basi kupitia picha hizi zitamfanya amtengee Allah wake japo dakika15 tu za kumkumbuka.